Matini Muhimu :
Home » » Mwenzangu

Mwenzangu

Imeandikwa na; Unknown mnamo, Jumanne, 17 Desemba 2013 | Jumanne, Desemba 17, 2013

Mwenza huyu simtaki, yu bado ang’ang’ania,
tena eti kahamaki, , hataki niachilia
Kama vile sina haki, kwa ninacho hitajia
Kajawa na taharuki, haki yangu kuijua
Mwanzo nilimrizia, kwa alivyo nidanganya
Sejua wake uzia, udugu kuuchanganya
sekuwa nikisinzia, hadaze zenikanganya
Hadi kuja nitanzia, alilotaka kufanya
Silaumu wangu baba, ambae kanipeleka
Hakufanya kisiriba, wasia aliuweka
He sema akinikaba, naweza kumuepuka
Ila naona msiba, amezidi kunishika
Ananivuta mashati, kila nikipapatuwa
Kuvuta hewa sipati, nihitajipo pumuwa
Tena ana tashititi, kejeli kajaaliwa
Kaniwekesha shariti, yutayari kuniuwa
(Mzalendo.net)
Sambaza hii :

Tafuta Kwenye Wikipedia

Matokeo ya utafutaji

 
Kwa Hisani ya : Muunda Blogu | Nawaje Ali | NAM
Fahari kwa Kiswahili Jukwaani
Hakimiliki © 2013 - 2018. Kiswahili Jukwaani - Haki Zote Zimehifadhiwa