Wenyewe ni wa Mwambao, Lugha hii Kiswahili
Walizusha babu zao, Tokea hivyo azali
Ikadumu hata leo, Yasemwa kila mahali
Lugha hii Kiswahili, Wenyewe ni wa Mwambao
Kuna kabila kusudi, Ambalo la Waswahili
Kuna hususa uludi, Ulijue jambo hili
Ukitaka yao jadi, Mwambao yao asili
Lugha hii Kiswahili, Wenyewe ni wa Mwambao
0 maoni:
Chapisha Maoni