CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU
AFRIKA MASHARIKI (CHAWAKAMA).
KATIBA YA AFRIKA MASHARIKI.
Tovuti: www.chawakama-am-webs.com
Barua pepe: chawakama2004@yahoo.com
“KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU”
.
CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU
AFRIKA MASHARIKI (CHAWAKAMA).
YALIYOMO:
SEHEMU YA KWANZA UKURASA
1.1. JINA LA CHAMA……………………………………………………… 2
1.2. WALEZI WA CHAMA………………………………………………… 2
SEHEMU YA PILI
2.0. MALENGO NA MADHUMUNI YA CHAMA………………………2
SEHEMU YA TATU
3.0. UANACHAMA NA ADA……………………………………… ………3
3.1. AINA ZA UANACHAMA……………………………………………. 3
3.2. HAKI ZA MWANACHAMA…………………………………………. 3
3.3. KIINGILIO NA ADA YA MWAKA…………………………………. 4
3.4. KUSITA UANACHAMA………………………………………………4
3.5. WAJIBU WA MWANACHAMA……………………………………...4
SEHEMU YA NNE.
4.1. MUUNDO WA UONGOZI.. ...…………………………………………... 5
4.2. MUDA WA UONGOZI……………………………………………...……5
4.3. MASHARTI YA UONGOZI………………………………………...……5
4.5. WAJIBU WA VIONGOZI…..…………………………………………….6
SEHEMU YA TANO.
5.0. FEDHA ZA CHAMA…………………………………………………….. 7
5.1. VYANZO VYA MAPATO………………………………………………..7
5.2. UWEKAJI, UCHUKUAJI WA FEDHA……………………….………….7
SEHEMU YA SITA.
6.0. VIKAO VYA CHAMA ………………………………………………….. 8
6.1. VIKAO VYA KAMATI KUU…………………………………………… 8
6.2. VIKAO VYA KAMATI YA UTENDAJI………………………………………..8
6.3. VIKAO VYA KAMATI YA NIDHAMU NA USIMAMIZI……………………9
6.4. MKUTANO MKUU WA CHAMA………………………………………………9
SEHEMU YA SABA
7.1.MABADILIKO YA KATIBA…………………………………………………….10
7.2. MRITHI WA CHAMA………………………………………………………...…10
.
CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU
AFRIKA MASHARIKI (CHAWAKAMA).
SEHEMU YA KWANZA
1.1. JINA LA CHAMA
Jina la chama ni CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI
VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI, Kwa kifupi-(CHAWAKAMA)
Makao makuu ni Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro
(MUM).
1.2. WALEZI WA CHAMA
Walezi wa chama katika Afrika mashariki.
1.2.1 Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI)-TANZANIA.
1.2.2 KENYA.
1.2.3 UGANDA.
1.2.4 RWANDA.
1.2.5 BURUNDI.
.
SEHEMU YA PILI.
20. MADHUMUNI YA CHAMA.
2.1. Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, na kukuza vipawa
vyao
2.1 Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya Kiswahili
2.2 kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Afrika Mashariki.
2.3 kushirikiana na vyama vingine vya Kiswahili katika juhudi ya kuendeleza
na kuimarisha lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Afrika Mashariki.
2.4 Kuunganisha wanafunzi wa lugha ya Kiswahili katika vyuo vikuu vya
ndani na nje ya Afrika Mashariki.
2.5 Kushirikiana na Asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji
wa Kiswahili Afrika Mashariki na Afrika yote kwa ujumla.
2.6 .Kuratibu makongamano ya mijadala mbalimbali inayohusu lugha ya
Kiswahili.
2.7 Kuchapisha jarida la CHAWAKAMA na machapisho mengine ili kukuza
taaluma ya Kiswahili.
2.8 Kubuni mikakati na mbinu za kuhimiza ukuzaji na uenezaji wa lugha ya
Kiswahili.
2.9 Kuweka kumbukumbu ya wataalamu kwa nia ya kuwatumia katika
kufanikisha malengo ya Chama na wahusika wa Kiswahili kwa ujumla.
SEHEMU YA TATU
3. UANACHAMA NA ADA.
Uko huru kwa mtu yeyote anayependa kujiunga na kutekeleza mambo yote
yanayohusiana na Chama kama kulipa kiingilio na ada, kuhudhuria vikao na
kushiriki katika kazi za kuiendeleza lugha ya Kiswahili.
Wanaoomba kujiunga na chama sharti wawe mwaka wa kwanza kwa shahada
ya uzamili.
Wanachama watakaojiunga mwaka wa tatu wa masomo yao watalipa ada ya
miaka yote mitatu iliyopita.
3.1 AINA ZA UANACHAMA
3.1.1. Uanachama wa kawaida.
.
(a) Wanachama waliochuoni.
Unawahusu Wanafunzi wote wanaosoma somo la Kiswahili katika Vyuo
Vikuu Afrika Masharikikwa kiwango cha shahada ya awali na shahada
Ya uzamili.
(b) Wanafunzi wasiosoma Kiswahili walio wazalendo wa lugha Kiswahili
Walioko Vyuo Vikuu Afrika Mashariki.
3.1.1.1.Wanachama walio Chuoni.
Unawahusu wanafunzi wote wanaosoma somo la Kiswahili katika Vyuo
Vikuu vya Afrika Mashariki katika kiwango cha shahada ya kwanza na
shahada za Uzamili.
3.1.1.2 Wanachama nje ya Chuo.
Unawahusu wote walio nje ya Chuo na waliohitimu masomo wakiwa
wanachama wa CHAWAKAMA.
Iwapo ataomba uanachama kwa kujaza fomu maalumu kutoka katika matawi
ya chama yaliyo hai.
3.1.2 Wanachama washiriki
Asasi zinazoshughulikia ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili zinaweza
kukubaliwa kuwa mwa anachama baada ya kuwasilisha maombi na
kukubaliwa na kamati ya utendaji ya Chama kwa kutimiza masharti
yatakayotolewa.
3.1.3 Uanachama wa Heshima
Hawa ni watu au taasisi ambazo kwa mchango maalumu wameonekana au
zimeonekana zinafaa Kupewa uanachama wa Heshima.
3.1.4 Uanachama wa wadhifa
Unawahusu walezi na wanataalamu wa somo la Kiswahili.
3.1.5 HAKI ZA MWANACHAMA.
Wanachama wote isipokuwa Wanachama Washiriki, Wanachama wa Heshima
na Wanachama wa Wadhifa watakuwa na haki zifuatazo:
3.1.5.1 .kupiga kura wakati wa uchaguzi.
3.1.5.2 . kugombea nafasi ya uongozi katika Chama kwa mujibu wa katiba hii.
3.1.5.3 .kuwasilisha hoja kwa ajili ya kujadiliwa katika Mkutano Mkuu.
.
3.3.0. KIINGILIO NA ADA.
3.3.1 Kila mwanachama atalipa kiingilio ambacho kitapangwa na Kamati ya Utendaji
na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu.
3.3.2 Kila mwanachama atatakiwa kutoa ada ya mwaka, kiasi ambacho kitapangwa
na kamati ya Utendaji na kuthibitishwa na Mkutano Mkuu.
3.3.3 Fedha zote katika kipengele(3.3.1) hapo juu zitakuwa katika mgawanyo
ufuatao:
Asilimia 30 itakwenda Afrika Mashariki, Asilimia 30 itakwenda Kanda na
Asilimia 40 itabaki tawini. Viwango hivi vitakuwa vikibadilika kulingana na
wakati.
3.4 KUSITA UANACHAMA.
Uanachama utasita kwa sababu zifuatazo:
3.4.1 Kutohudhuria mikutano ya chama mara tatu mfululizo bila ya taarifa na sababu
za kuridhisha.
3.4.2 Kutolipa ada ya mwaka kwa muda wa miaka miwili mfululizo.
3.4.3 Kujiuzulu uanachama.
3.4.4 Kufukuzwa au kuachishwa uanachama na Mkutano Mkuu kwa kura
zisizopungua robo tatu ya wajumbe waliohudhuria.
3.4.5 Kifo cha mwanachama.
3.4.6 Kutokuwa katika hali ya akili timamu.
3.5.0 WAJIBU WA MWANACHAMA
3.5.1 Kueneza na kukuza lugha ya Kiswahili.
3.5.2 Kulipa ada na michango mingine
3.5.3 Kutoa maoni juu ya mwenendo wa chama ili kukiimarisha chama.
3.5.4 Kukuza kipaji chake kwa kupitia majarida na makala mbalimbali
3.5.5 Kugombea nafasi za uongozi.
3.5.6 Kuchagua viongozi
3.5.7 Kuhudhuria vikao vya chama
SEHEMU YA NNE.
4.1 UONGOZI
4.1.1 CHAWAKAMA Afrika Mashariki Viongozi watakuwa:
.
Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti,Katibu Mkuu, Naibu Katibu, Mweka
Hazina, Mweka Hazina Msaidizi, Afisa Uhusiano, Afisa uenezi, Mhariri
Mkuu na Mhariri Msaidizi.
4.1.2 Viongozi wa CHAWAKAMA Afrika mashariki watachaguliwa kulingana
na mgawanyo wa nafasi za uongozi, na watapitishwa na Mkutano Mkuu wa
chama wa Afrika Mashariki.
4.1.3 Kwa kadri inavyowezekana nafasi za uongozi wa Chama zitagawanywa
sawa kwa Kanda na matawi husika katika Kanda isipokuwa Katibu Mkuu
atatoka yalipo Makao Makuu ya Afrika Mashariki.
4.1.4 Wenyeviti na makatibu wa kanda ni wajumbe wa kamati ya utendaji ya
Afrika Mashariki.
4.1.5 Kutakuwa na kamati ya Nidhamu na Usimamaizi ya Afrika mashariki.
(kamati itakuwa na Mwenyekiti na Katibu)
4.1.6 Kamati ya Nidhamu na Usimamizi wa kanda itaundwa na wajumbe watano
ambao watateuliwa na kamati ya utendaji ya kanda husika katika kikao cha
kwanza.
4.2 MUDA WA UONGOZI.
4.2.1 Kamati ya Utendaji itakuwa madarakani kwa muda wa mwaka mmoja,Wajumbe wa
Kamati wanaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine kisichozidi miaka miwili
isipokuwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Mhazini ambao wataongoza kwa mwaka
mmoja tu na nafasi zao kupokelewa na Makamu au Manaibu wao.
4.2.2 kamati ya Nidhamu na usimamizi itakuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu
tangu tarehe ya uteuzi.
4.3 MASHARTI YA VIONGOZI.
Kiongozi anatakiwa:
i. Kuwajibika kwa mujibu wa Katiba.
ii. Kuhudhuria vikao vyote vya Chama.
iii. Kutunza mali na hadhi ya Chama.
iv. Kutotoa na kupokea rushwa.
v. Kujiuzulu anapoona kazi imemshinda.
.
vi. Kukubali kuwajibika.
4.4 WAJIBU WA VIONGOZI.
4.4.1 Mwenyekiti.
i. Msimamizi mkuu wa shughuli za Chama.
ii. Msemaji mkuu wa Chama.
iii. Mwongoza mikutano ya Chama (Kamati Kuu na Mkutano Mkuu)
iv. Kiongozi wa misafara ya Chama.
v. Kusimamia nidhamu ya viongozi.
4.4.2 Makamu wa Mwenyekiti.
i. Msaidizi Mkuu wa Mwenyekiti.
ii. Mwenyekiti wa vikao vyote vya Chama kama Mwenyekiti hayupo.
iii. Msaidizi na Mshauri wa Mwenyekiti.
iv. Kufanya kazi nyingine atakazoagizwa na Mwenyekiti.
4.4.3 Katibu Mkuu.
i. Mtendaji Mkuu wa Chama.
ii. Mtunza kumbukumbu za Chama.
iii. Mtunza mali ya Chama.
iv. Katibu wa mikutano ya Chama.
v. Kuitisha vikao.
vi. kuidhinisha matumizi ya fedha za Chama.
vii. Kuratibu shughuli za Chama.
viii. Kutoa ripoti juu ya maendeleo ya Chama.
ix. Kutunza orodha ya wanaChama.
x. Kutunza mihuri ya Chama.
4.4.4 Katibu Msaidizi.
i. Msaidizi wa Katibu Mkuu
ii. Mshauri wa Katibu Mkuu
iii. Kufanya kazi zote za Katibu Mkuu wakati hayupo
iv. Kufanya kazi nyingine atakazoagizwa na Katibu Mkuu
4.4.5 Mweka Hazina.
i. Atakuwa mdhibiti mkuu wa fedha na mali za Chama.
.
ii. Atahakikisha kuwa kuna mfumo mzuri wa kupokea, kudhibiti na kulipa fedha
za Chama.
iii. Atatengeneza makisio ya mapato na matumizi ya Chama
iv. Atafanya malipo kwa kufuata taratibu na kanuni za fedha zilizowekwa
v. \Atakuwa mweka saini wa lazima katika akaunti za benki za Chama
vi. \Ataandika na kutunza vitabu vya hesabu ya Chama
vii. \Atatayarisha hesabu na taarifa za fedha za mwaka na kuziwasilisha kwa
kamati ya utendaji kabla ya kuwasilisha katika Mkutano Mkuu .
viii. Atatunza na kudhibiti mali na raslimali za Chama
ix. Atahakikisha kuwa kila mwisho wa mwaka wa fedha, mali yote inahakikiwa.
4.4.6 Mweka Hazina Msaidizi.
i. Atamsaidia mweka hazina kudhibiti fedha na mali za Chama
ii. Kusaidia kuhakikisha kuwa kuna mfumo mzuri wa kupokea, kudhibiti na
kulipa fedha za Chama.
iii. Kusaidia kutengeneza makisio ya mapato na matumizi ya Chama
iv. Kusaidia kufanya malipo kwa kufuata taratibu na kanuni za fedha
zilizowekwa
v. Atafanya kazi zote atakazoagizwa na Mweka Hazina Mkuu pamoja na
Mwenyekiti.
4.4.7 Afisa Uhusiano.
i. Atabuni na kuratibu mipango ya ushirikiano miongoni mwa nchi na asasi
wanachama
ii. Kutembelea asasi wanachama ili kufuatilia shughuli za Chama
iii. Katika utekelezaji wa majukumu haya, Afisa uhusiano atashirikiana kwa karibu na
Katibu na Makamu Mwenyekiti, Naibu katibu, na Mhariri Mkuu.
4.4.8 Afisa Mwenezi.
Atasimamia utangazaji na uenezi wa shughuli za Chama ili kuleta mahusiano mema
na maelewano na umma, Vyombo vya Habari, Serikali, Mashirika ya uhisani na
asasi nyinginezo.
4.4.9 Mhariri Mkuu.
i. Atasimamia na kuratibu uandaaji, uhariri na utoaji wa jarida la Chama
pamoja na vitabu., Machapisho hayo yanaweza kuwa katika umbo la
karatasi au la elektroniki.
ii. Atakuwa ndiye mratibu mkuu wa masuala ya ushirikiano katika uchapishaji
na ubadilishaji wa machapisho.
.
5.0 Kamati ya Nidhamu na Usimamizi.
i. Itasimamia nidhamu ya viongozi wote wa kanda .
ii. Itapokea na kushughulikia matatizo/migogoro itakayojitokeza ndani ya
uongozi kwa kushirikiana na Mlezi wa Chama.
iii. Itashirikiana na Uongozi juu ya uendelezaji wa shughuli za chama.
SEHEMU YA TANO
5.1 FEDHA ZA CHAMA
5.1.1 Vyanzo vya mapato
Mapato ya Chama ni;
5.1.2 Kiiingilio na Ada ya mwaka ya kila mwanaChama
5.1.3 Misaada, zawadi au ruzuku kutoka kwa wafadhili, wanachama, wahisani, watu
binafsi na vyombo vingine.
5.1.4 Mapato yatokanayo na shughuli mbalimbali au miradi ya Chama
5.1.5 Fedha itokanayo na mikopo
5.1.6 Mwanachama au mfadhili yeyote wa Chama anaweza kutoa fedha au kukisaidia
Chama kwa njia yoyote atakayoona inafaa.
5.2 Uwekaji, uchukuaji wa fedha za chama.
5.2.1 Fedha za Chama zitawekwa katika benki itakayoteuliwa na Kamati ya
Utendaji.
5.2.2 Kutafunguliwa akaunti mbili katika benki;
5.2.2.1 Akaunti ya matumizi ya kawaida
5.2.2.2 Akaunti ya mfuko wa maendeleo wa ukuzaji na uenezi wa
lugha.
.
5.2.3 Watia saini
5.2.3.1 Mwenyekiti wa Afrika Mashariki
5.2.3.2 Katibu wa Afrika Mashariki
5.2.3.3 Mhazini wa Afrika Mashariki
5.2.3.4 Katibu wa kamati ya Nidhamu na Usimamizi ya Afrika Mashariki.
Kamati Kuu itaandaa utaratibu wa kuchukua fedha benki
SEHEMU YA SITA
6.0 VIKAO VYA CHAMA
6.1 Kamati kuu
6.1.1 Wajumbe wa kamati kuu
Viongozi wote waliopitishwa na mkutano mkuu wa Afrika Mashariki.
6.1.2 Akidi: Nusu ya wajumbe wote
6.2 Kazi za kamati kuu
6.2.1 Kutafuta vyanzo vya mapato
6.2.2 Kutengeneza na kuratibu sera za Chama
6.2.3 Kuandaa programu ya shughuli za Chama
6.2.4 Kuangalia maendeleo ya Chama
6.2.5 Kusimamia shughuli za Chama
6.2.6 Kutoa mapendekezo ya Chama na kusimamia utekelezaji wake
6.2.7 Kuunda kamati mbalimbali za utendaji kutegemeana na uhitaji
6.2.8 Kusimamia ajenda za Mkutano Mkuu
Idadi ya vikao vya kamati kuu vitafanyika mara mbili kwa mwaka. Aidha
Vikao vya dharura vitakuwepo endapo vitahitajika.
6.3 Kamati ya utendaji
Kamati itakuwa na vikao viwili kwa mwaka
Kamati ya utendaji itajumuisha Mwenyekiti, Makamu mwenyekiti ,Katibu,
Naibu katibu, Mhazini, Mhazini Msaidizi wa kanda, na Wenyeviti wote wa
Matawi.
6.4 Kamati ya Nidhamu na Usimamizi ya kanda
.
Itafanya vikao vyake kulingana na majukumu ya wakati husika.
6.4 Mkutano Mkuu wa Chama
6.4.1 Wajumbe wa mkutano Mkuu
Ni wanaChama wote
6.4.2 Akidi theluthi moja (1/3) ya wanaChama wote
6.4.3 Kazi za Mkutano Mkuu wa kanda.
Kupitisha mapendekezo ya kamati
Kupokea taarifa ya kamati
Kutoa ushauri katika uendeshaji wa Chama
6.5 Idadi ya vikao vya Mkutano Mkuu.
Mkutano Mkuu utafanyika mara moja kwa mwaka na vikao vya
dharuravitafanyika iwapo vitahitajika. Mkutano mkuu wa Afrika Mashariki
utaambatana na kongamano la Afrika Mashariki.
CHANZO: CHAWAKAMA MUM
1 maoni:
Nisaidieni namna ya kujiunga ndugu zangu
Chapisha Maoni