BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI
YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25 Februari, 2014
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI
YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Baraza la Mitihani la
Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa
matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa
baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la
Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:
1.
Viwango vya ufaulu
(grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa
wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo
katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua
namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo
husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5)
kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia
utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo
ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano
mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama
inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali
Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana
kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili
(12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria,
Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
2.
Kwa kuzingatia
viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali
na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni
Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na
kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo
husika.
3.
Madaraja ya ufaulu
yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza
kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla
ya alama (Points) na Ufaulu katika Daraja
la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi
D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya
Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana
kwenye Jedwali la 2.
Jedwali 2: Madaraja
yaliyotumika katika CSEE 2013
4.
Kwa mujibu wa Kanuni
za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit”
na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za
kufeli.
5.
Baraza la mitihani la
Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na
mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa
na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
Chanzo www.necta.go.tz
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Madaraja na Viwango vya Ufaulu Kidato cha 4
Imeandikwa na; Unknown mnamo, Alhamisi, 27 Februari 2014 | Alhamisi, Februari 27, 2014
Lebo:
soma
0 maoni:
Chapisha Maoni