Matini Muhimu :
Home » » Safari ya Wanafunzi wa CHAWAKAMA Bagamoyo

Safari ya Wanafunzi wa CHAWAKAMA Bagamoyo

Imeandikwa na; Unknown mnamo, Jumatano, 8 Januari 2014 | Jumatano, Januari 08, 2014


SAFARI YA BAGAMOYO YAFANA
Tarehe 14/11/2013 ilikuwa ni historia kwa wanachama wa chawakama pamoja na Waraibu wa lugha ya kiswahili. Ilikuwa ni siku adhimu baada ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ya mji wa bagamoyo kutoka Chuo kikuu cha Waislamu Morogoro.Jumla ya watu waliojumuika katika safari ile walikuwa ni 105 wakiwemo wakufunzi na viongozi wa Tawi na Afrika Mashariki.Safari ilianza saa 1:00 asubuhi, tukipita maeneo tofauti tofauti kama Chalinze,Msoga,Mboga na vijiji vingine vya mkoa wa Pwani.Saa 11:15 asubuhi gari liliingia katika mji wa Bagamoyo Moja kwa moja safari yetu ilianzia katika Taasisi ya sanaa Bagamoyo.Tulipowasili wenyeji wetu walitukaribisha na mara baada ya taratibu za kiuongozi kukamilika tulianza kuzuru katika maeneo tofauti tofauti katika Taasisi hiyo.Kwanza tulianza kutembelea katika eneo la sanaa za mikono ikiwemo uchoraji na ufinyanzi.Hapo tulijifunza mambo kadhaa yanayohusiana na hii fani.Baada ya hapo tuliekea katika kitengo cha sanaa za maeonesho kitengo cha uandaaji wa majukwaa.Hapo tulipata maelezo mengi yanayohusiana na uandaaji wa majukwaa katika hii michezo ya kuigizo.Tulipomaliza wenyeji walitukaribisha katika ukumbi wa mikutano ambapo mkufunzi wa Chuo hicho Mzee Abdurahmani(Maaalim Bulla) alitupa maelezo mafupi juu ya uandaji wa tamthiliya.Saa 15:00mchana tulimaliza na wanachama kupata chakula.Mapumziko mafupi yalifuata kisha kuanza safari ya kwenda kwenye magofu ya kaole.Hapo tulijifunza mambo mengi ya kuvutia na kustaajabisha.Safari haikuishia hapo bali wanachama walikwenda Kaole Crocodile Ranch kujionea mamba wa kufuga.Hatma za Matembezi ndani ya Bagamoyo yalikuwa ndani ya soko la samaki.Wanachama walipata kununua samaki mbalimbali wanaopatikana ndani ya Bahari ya Hindi.Saa moja kamili usiku safari ya kurejea Morogoro ilianza na saa nne ya usiku tuikuwa tumefika Morogoro tukiwa tumechoka lakini wenye furaha tele na kila aliyeenda alibaki kusimulia mazuri aliyojionea.Hizi ni juhudi za Viongozi,mlezi na Wanachama kwa ujumla katika kuhakikisha vizuri tunavienzi na kuvithamini haswa utamaduni wetu Waswahili na kiswahili kwa ujumla.Tumshukuru Mwenyeezi Mungu kwa kutupeleka salama na kuturudisha salama.
KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU.



Hapa msafaya ulikutana na foleni

mmmh!

Wanachama walipata kupata upepo wa bahari

Hapa Mkufunzi akitoa maelekezo kuhusu sanaa ya uchoraji

Wanachama wakisikiliza kwa makini

Hapa wakipokea mafunzo kuhusu uandaaji wa jukwaa

Moja ya majukwaa ya kuigizia

Sehemu ya jukwaa kubwa tasuba

moja ya sanamu lililotengezwa kwa sementi

Mwenyekiti akitoa maelezo mafupi ya msafara kwa wenyeji

Maalim Bura akitupa somo kuhusu tamthiliya

NDANI YA MAGOFU YA KAOLE




Hapa tukitazama Mamba

wanachama wakiingia ndani ya soko la samaki

CHANZO CHAWAKAMA MUM
Sambaza hii :

0 maoni:

Tafuta Kwenye Wikipedia

Matokeo ya utafutaji

 
Kwa Hisani ya : Muunda Blogu | Nawaje Ali | NAM
Fahari kwa Kiswahili Jukwaani
Hakimiliki © 2013 - 2018. Kiswahili Jukwaani - Haki Zote Zimehifadhiwa