Matini Muhimu :
Home » » Mtoto wa Mbu

Mtoto wa Mbu

Imeandikwa na; Unknown mnamo, Jumatano, 19 Februari 2014 | Jumatano, Februari 19, 2014

Mtoto wa mbu alitoka nje ya nyumba yao, akijifunza kupaa kwa mara ya kwanza. Aliporudi baba yake, akamwambia "Hongera sana mwanangu, unajisikiaje ulipopaa? Mtoto kajibu "Najisikia furaha sana! Maana kila nilipokuwa napita watu walikuwa wananipigia makofi" Mama yake akamwambia "Sio makofi ya pongezi hayo mwanangu! Kila walipopiga makofi walitaka wakuuwe!.

TANBIHI

Si kila anaye kufurahiya au kukupigia makofi kuwa anakupenda na kukulakia kila la heri bali wengine ni wanafiki na adui zako kuwa makini na hilo!
Sambaza hii :

0 maoni:

Tafuta Kwenye Wikipedia

Matokeo ya utafutaji

 
Kwa Hisani ya : Muunda Blogu | Nawaje Ali | NAM
Fahari kwa Kiswahili Jukwaani
Hakimiliki © 2013 - 2018. Kiswahili Jukwaani - Haki Zote Zimehifadhiwa