UTENZI WA CHAWAKAMA
SIKU YA
KISWAHILI
CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO
1. NAANZA KWA
LAKE JINA,
MTUKUFU SUBUHANA,
ALIYETANDIKA SAMA,
BILA NGUZO KUZUIA.
2. NI YEYE
ALOMILIKI,
KAENEZA KWA MALAKI,
WALA HANA MSHIRIKI,
KATIKA HII DUNIA.
3. SALAMU
ZENYE HAMASA,
ZENDE KWA WETU AFISA,
BAKARI SADANI HASA,
ELIMU KUSHIKILIA.
4. SALAMU NI
KUSALIMU,
WEWE NI WETU MWALIMU,
ASALAMU ALAYKUMU,
KARIBU NINAKWAMBIA,
5. KARIBU MGENI
WETU,
KATIKA HAFLA YETU,
KISWAHILI LUGHA YETU,
NDIO TUNAJIVUNIA.
6. NA WAGENI
MASHUHURI,
MLOIFUNGA SAFARI,
VYOTE MKAWA TAYARI,
KUUNGANA KWAPAMOJA.
7. KARIBUNI
TWAWAAMBIA,
SALAMU TWAWAPATIA,
HESHIMA KWENU TWATOA,
MKONO NAWAPUNGIA.
8. WANACHAMA
CHAWAKAMA,
MUNGU AWAPE SALAMA,
NAONA MMERINDIMA,
NYOTE MMEHUDHURIA.
9. BAADA DIBAJI
HIYO,
NISEME TULIONAYO,
HILO TENA KUSUDIO,
LEO HII TUKAMEYA.
10. NI SIKU YA
KISWAHILI,
KWA MWAKA SI MARAMBILI,
HILO NISEME UKWELI,
NYOTE MPATE UJUA.
11. NI MARA MOJA
KWA MWAKA,
SIKU HII KUSIKIKA,
MAMBO MENGI TAFANYIKA,
NYOTE MTAJIONEA.
12. TWACHAKATA
KISWAHILI,
KWA SHUGHULI MBALIMBALI,
LUGHA IWE MUHIMILI,
HAPA PETU TANZANIA.
13. TUTUMIE
LUGHA YETU,
NDIO AZIMIO LETU,
HUYU NDIE MWANA KWETU,
WAJIBU NI KUMLEA.
14. TUKIENZI
KISWAHILI,
KIWEZE PIGWA MITHILI,
NDANI MWETU BARA HILI,
NA KOTE KWENYE DUNIA.
15. LENGO LENYE
MSHAWASHA,
NCHI KUISWAHILISHA,
KISWAHILI KUWA KASHA,
KILA NGAZI KUTUMIA.
16. KISWAHILI
KIWE JUU,
HILI NDILO LENGO KUU,
NGAZI ELIMU YA JUU,
NA KONA ZOTE PAMOYA.
17. HEBU NYOTE
FIKIRINI,
NCHI ZA UGHAIBUNI,
METUMIA LUGHA GANI,
NDIO WAKAENDELEA.
18. UKIENDA KWA
UNDANI,
LUGHA ZAO ZA NYUMBANI,
WACHINA NA MAREKANI,
NDIZO WALIZOTUMIA.
19. KWA KWELI
YASIKITISHA,
TAMAA INA KATISHA,
LUGHA YETU TWAIFISHA,
HIYO INA YOYOMEA.
20. HIYO INAYOYOMEA,
DUNIANI YAPOTEA,
SOTE WAZUNGU MEKUA,
KISWAHILI NI UDHIA.
21. TUPANGENI
MIKAKATI,
KIWEZE KUPANDA CHATI,
UKUTA WA KANGRITI,
SOTE TUNGEJIJENGEA.
22. KWENU
NYINYI MAAFISA,
HILI NDIYO LENGO HASA,
MNAPO PATA FURUSA,
NIVYEMA MKATETEA.
23. NANYI WETU WAHADHIRI,
NYOTE MUWEPO TAYARI,
TUZIONDOSHE DOSARI,
ZOTE ZINOTOKEZEA.
24. TUJENI KWA
WANAFUNZI,
LUGHA YETU TUIENZI,
HAPO TUTAPANDA NGAZI,
KILELENI TUTAKUA.
25. CHAWAKAMA
TUSILALE,
NATUWE KUMBELEMBELE,
DONDA LIKIOTA NDWELE,
KWA KWELI TUTAUMIA.
26. HONGERENI
CHAWAKAMA,
NYOTE KUSIMAMA WIMA,
TWAWAOMBEA SALAMA,
CHAMA KIZIDI KUMEA.
27. CHAMA
KUKIENDELEZA,
VIZURI KINATUFUNZA,
NAOMBA KIWE CHAKWAZA,
HILI KULIANGALIA.
28. NITAKUWA MTU DUNI,
KWA NYOTE MLIYO NDANI,
KAMA SIJAWAMBIENI,
VIGOGO WANOKILEA.
29. WALEZI WA
CHAMACHETU,
WAKWANZA MWALIMU WETU,
MZEE KONDO NI WETU,
CHAMA KAKISHIKILIA.
30. NA ALHAJI
TAMIMU,
WENGI MNAMFAHAMU,
AYABEBA MAJUKUMU,
KATIKA CHAKE KIFUA.
31. UKIJA KWA
WAHADHIIRI,
HAPA KWAKWELI NI SHWARI,
HEBU CHEKI MANDHARI,
LEO ILIYOVYOTULIA.
32. MWALIMU WETU
HAMADI,
KWAKWELI NI MARIDADI,
SIO JOTO SI BARIDI,
YEYE KWAKE MAMBO POA.
33. NA BI FATUMA
KAWALE,
BI KHADIJA VILE VILE,
NAWAJE NAE YU PALE,
KITINI AMETULIA.
34. MWALIMU WETU
PONERA,
YEYE HANA MASIHARA,
KONGAMANO LIWE MARA,
MICHANGOYE ATATOA.
35. KIVULI MVUMO KAKA,
MKE NAMPA TALAKA,
KWAKWELI NA BURUDIKA,
SHAIRI NIKIPITIA.
36. BWANA AHMEDI
SOVU,
CHAWAKAMA N I MWEREVU,
CHAMA HAKIFANYI KOVU,
MCHANGO WAKIPATIA,
37. KAKA YETU
SELASELA,
SIIJUI YAKO ILA,
CHAWAKAMA NICHAKULA,
KUKIKOSA NI UDHIA.
38. NI SAFU YA
VIONGOZI,
CHAWAKAMA KILA NGAZI,
HAWA NDIO WAPAGAZI,
MZIGO WAJIBEBEA.
39. KATIBU WETU
MIKIKI,
AFRIKA MASHARIKI,
JUMBE UMESTAHIKI,
HONGERA NAKUPATIA.
40. MWENYEKITI
CHAWAKAMA
MATIBWA HEBUSIMAMA
KATIBU USIWENYUMA
KIULA NAKUNGOJEA.
41. KAMATI YETU
YA FEDHA,
TAKATO AMEIWEZA,
BAJETI AKITANGAZA,
NYOTE MTAFURAHIA.
42. NA VIONGOZI
WENGINE,
KWA PAMOJA NIWANENE,
ITIFAKI
NISIKANE,
NYOTE
MNGESALIMIA.
43. AWABARIKI
MWENYEZI,
MUZIFANYE VYEMA KAZI,
MUEPUKE
VIZUIZI,
MOLA
ATAJAALIA.
44. TUNA NYINGI
CHANGAMOTO,
NI KUBWA SI ZAKITOTO,
KWA
KWELI ZATUPA JOTO,
UNYONGE
ZINATUTIA.
45. VIPIGA CHAPA
KIPATA,
KWAKWELI MOYO TATUTA,
HI
VI VYOTE KIVILETA,
CHAMA
CHETU TAPUMUA.
46. ATUJALIE
MANANI,
TUIFUZU MITIHANI,
YASIRI
NA HADHARANI,
MUNGU
ATONGOZE NJIA.
47. AMPE WETU
SADANI,
HURUMA KWAKE MOYONI,
AWE
WA KWETU MGENI,
MAHAFALI
KIFIKIA.
48. NASRA WENU
FUADI,
MGHANI NILORADIDI,
MALENGA
ALI HAMADI,
CHAWAAKAMA
TWATOKEA.
0 maoni:
Chapisha Maoni